Umuhimu wa mazao ya misitu yasiyo miti kwa Uhakika wa chakula katika kaya za Tanzania
Loading...
Date
2000-07
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO
Abstract
Uhakika wa chakula limekuwa ni suala muhimu katika mijadala mbalimbali ya sera za kuondoa
umasikini katika nchi nyingi zinazoendelea. Licha ya ongezeko kubwa la uzalishaji wa chakula
katika nchi mbalimbaliwatu milioni 790 katika nchi zinazoendelea wanakabiliwa na uhaba wa
chakula. Pia watu milioni 34 walioko kwenye nchi zenye viwanda na nchi zenye maendeleo ya
kati wana uhaba mkubwa wa chakula (FAO 1999a). Kama watu wote wasio na lishe ya kutosha
wangewekwa pamoja, idadi yao ingekuwa kubwa kuliko bara lolote lile ukiacha bara la Asia
(FAO 1999a).
Description
Jarida
Keywords
MAZAO YA MISITU, CHAKULA KATIKA KAYA, ELIMU YA JINSIA